Miradi ya Mazingira
Kazi Zetu nchini Tanzania

Miradi ya
Kimkakati

Tunatekeleza miradi endelevu inayolenga kuleta mabadiliko chanya ya kijamii, kiuchumi na mazingira.

Nyanja Tunazozifanyia Kazi

Our Core Projects

Uhifadhi wa Mazingira

Tunashughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo nchini Tanzania. Kupitia kampeni zetu za "Ziara Yangu, Mti Wangu" na "Shitaka Urithi Mazingira", tunahamasisha upandaji miti endelevu na utunzaji wa mazingira.

Soma Miradi Iliyotekelezwa

Msaada wa Kisheria & Uraia

Tunatoa elimu thabiti ya uraia, haki za binadamu na utawala bora. Taasisi inajikita katika kutoa msaada wa kisheria na ushauri wa bure kwa makundi ya jamii wasio na uwezo au walio katika mazingira magumu ili kuhakikisha usawa vya haki.

Soma Maelezo ya Idara

Uwezeshaji Kiuchumi

Kupitia mafunzo ya ujuzi wa kazi na ujasiriamali, tunalenga kuamsha fikra chanya (mindset change) kwa vijana na wanawake ili kuwawezesha kuanzisha mitandao imara ya biashara, kukuza vipato na kujenga fursa za ajira endelevu.

Soma Maelezo ya Idara

Maendeleo ya Jamii

Tunasimamia midahalo, makongamano na mafunzo maalum. Kupitia jukwaa letu la "Wito Wa Kunyanyuka" tunajenga jamii yenye fikra chanya na yenye kuchukua hatua za kimaendeleo kwa vitendo.

Soma Miradi Iliyotekelezwa
Inua Jamii, Tunza Kesho

Ungana Nasi Kuleta Mabadiliko

Kila mchango wako una nguvu ya kubadilisha maisha, kuwezesha jamii kiuchumi, na kulinda urithi wa mazingira yetu. Kuwa sehemu ya safari hii ya maendeleo leo.